Sauti na kilio cha Mwanainchi



Ni siku mingi nimekuwa nikisema mimi ni mzalendo..
Kwa nchi ambayo imejawa na maisha ya magendo..
Hakuna upendo..
Maisha ni ya utengano..
Nchi ambayo imejawa na ukabila...
Wengine wameishikilia ni kaa kwao ni mila..
Ama lengo lao ni nchi kubaki bila...
Niko kwa ile nchi ambayo viongozi wanatuona kama sanamu..
Tena Baada ya kuingia kwa ule utamu..
Bila kutambua tuliwamwagia damu..
Tena si ya mnyama bali ya wenzetu binadamu..
Baada ya miaka tano Wanarudi kutubembeleza..
Wakituelezea zao sera..
Wakituhonga na zao hela...
Wakisema ati..
"yaliopita si ndwele,maisha ni kusonga mbele"
Ilhali Maendeleo kwao ni kama panya kumfunga paka kengele..
Niko kwa nchi ambayo viongozi hawaaminiki..
Na sauti ya mwanainchi haisikiki ...
Niko kwa ile nchi ambayo kazi ni kwa vijana..
Lakini mshahara ni kwa wazee..
Nchi ambayo jogoo akiwika anachinjwa
Na mambo yake yanafichwa
Ni wengi wetu hawana amani...
Na ni wachache wetu waimeishiwa na imani..
Kwamba ipo ile siku tutakuwa na uhuru..
Na itakuwa lazma tu kama kulipa ushuru..
To be continued......
#ApieceOfMindArt..

Comments

Popular posts from this blog

Dear Dad & Mum

"Dance With Me"

Infatuation.